email us at
info@ntlp.go.tz
call us now

+255 (0) 26 2960150

Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma - Taarifa Muhimu

Kwakuwa Tanzania inakabiliana na janga la COVID-19, ni muhimu kuhakikisha kuwa huduma muhimu na mikakati ya kushughulikia magonjwa mengine ya kuambukiza zinadumishwa. Kwa mtazamo huu, juhudi za kuwatafuta wahisiwa wa ugonjwa wa Kifua kikuu, na matibabu ni muhimu ziendelee. COVID-19 imeonyesha changamoto katika udhibiti wa TB kwani magonjwa yote yanaathiri mapafu na dalili zinashaabiana. Hii imewawia vigumu watoa huduma katika vituo vya kutolea tiba na kusababisha uwoga na hata sintofahamu.

Utangulizi

Kwakuwa Tanzania inakabiliana na janga la COVID-19, ni muhimu kuhakikisha kuwa huduma muhimu na mikakati ya kushughulikia magonjwa mengine ya kuambukiza zinadumishwa. Kwa mtazamo huu, juhudi za kuwatafuta wahisiwa wa ugonjwa wa Kifua kikuu, na matibabu ni muhimu  ziendelee.

COVID-19 imeonyesha changamoto katika udhibiti wa TB kwani magonjwa yote yanaathiri mapafu na dalili zinashaabiana. Hii imewawia  vigumu watoa huduma katika vituo vya kutolea tiba na kusababisha uwoga na hata sintofahamu. 

 Ulinganisho wa dalili za TB na COVID-19

 

 Vipengele muhimu  

 

Kifua Kikuu

 

COVID-19

 Jinsi inavyoenea

 husambazwa kwa njia ya hewa  husambazwa kwa njia ya majimaji  

 Ugunduzi

 

 Vipimo vya makohozi kwa wale walio na kikohozi. Sampuli zingine kulingana na dalili

 Vipimo vya maji maji puani (Nasal swab) au vipimo vya makohozi

 Mdudu anayeeneza  Mycobacterium  tuberculosis complex   Severe acute respiratory syndrome coronavirus 2 (SARS-CoV-2)  
 Maambukizi

 Kadirio la chini ya mtu1 hadi watu 4 wanaweza kuambukizwa na mtu mmoja mwenye TB

 Hivi sasa wastani wa watu 2.2 wanaweza kuambukizwa  na mtu mmoja aliye na COVID-19

 Namna ya kuzuia  Hatua za kuzuia ni pamoja na tiba ya kuzuia Kifua kikuu kwa wale walio na karibu na mgonjwa wa TB na kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa na kupiga chafya

Kukaa kwa umbali wa mita moja au mbili kati ya mtu na mtu, Kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa na kupiga na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kwa angalau sekunde 20

 Matibabu  Dawa  za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa miezi 6 na kifua Kikuu sugu kwa miezi 4-24  Kwa sasa ni matibabu kulingana na dalili zinazojitokeza. Kuna matumizi ya dawa za majaribio kwa wakati huohuo
 Chanjo  BCG kwa watoto chini ya miaka 5 inazuia TB kali  Tafiti zinaendelea

 

Nini kifanyike?

1. Watoa huduma katika vituo na ngazi ya jamii kupewa elimu ya kutofautisha dalili za TB na zile za COVID-19. Hii ikiwa ni pamoja na wataalamu wa maabara.

2. Kuongeza muda na kugawa makundi kwa wagonjwa wanaokuja kliniki ili kuepuka msongamano.

3. Wagonjwa wenye historia nzuri ya utumiaji wa dawa kupatiwa dawa zaidi ya wiki mbili, kwa wale walio katika awamu ya kwanza (intensive phase) na wale walio katika awamu ya pili (continuation phase) wapatiewe wapatiewe dawa za mwezi mzima.

4. Watoa huduma wanaohudumia vituoni na kwenye jamii, kupatiwa vifaa vya kujikinga na maambukizi kama vile barakoa.

5. Kufanya ufuatiliaji wa wateja wanaojifanyia uchunguzi kwa kutumia mtandao wa simu wa TAMBUA TB