Phone: +255 (0) 26 2960150 | Email: info@ntlp.go.tz
Home / Media / Blog / Gharama za Fedha isiwe Kikwazo Kwa Wagonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma Kupata Matibabu

Gharama za Fedha isiwe Kikwazo Kwa Wagonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma Kupata Matibabu

image

GHARAMA ZA FEDHA ISIWE KIKWAZO KWA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU NA UKOMA KUPATA MATIBABU.

Na. NTLP- Dodoma.

Mpango wa utekelezaji wa hifadhi ya jamii kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma nchini unalenga kusaidia wagonjwa wa TB na Ukoma kupata huduma pasipo kuingia gharama zozote. Mpango huu pia unaenda sambamba na mikakati ya Wizara ya Afya ambayo inaelekeza Wadau wote wanaohusika na utoaji huduma za Kifua Kikuu na Ukoma kusaidia na  kuondoa gharama za matibabu kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma nchini.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Meneja Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma Dkt Riziki Kisonga alipokuwa akifungua kikao kazi cha awali kwa ajili ya uandaaji wa Mpango wa hifadhi ya jamii kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma nchini Jijini Dodoma.

“Tunatamani mgonjwa yoyote wa Kifua Kikuu toka siku anagunduliwa mpaka anapomaliza matibabu yake, gharama za fedha isiwe kikwazo katika kupata huduma za Kifua Kikuu na Ukoma” alisema.

Mpango huu unakuja kutatua tatizo hili kwa kutoa maelekezo nini kifanyike katika ngazi zote ambazo mgonjwa anatakiwa kupata huduma sambamba na kuimarisha mifumo mingine ya huduma za lishe, ufuasi wa dawa, huduma za uchunguzi pamoja na kumjengea uwezo mgonjwa juu ya namna bora ya kujitegemea kwa kuwa na shughuli za kufanya na kumuingizia kipato ili aweze kujikimu kimaisha.

Naye, Mtalaamu mshauri anayeratibu utengengenezaji wa Mpango wa Hifadhi ya Jamii Bw. Jeddy Mzungu alieleza umuhimu wa mpango huu katika mapambano dhidi ya kifua kikuu nchini ambapo alibainisha mpango huu utaenda kuwasaidia wagonjwa kuwakinga na madhira mbalimbali wanayoweza kuyapata kiuchumi na kijamii  kutokana na ugonjwa wa TB.

“Wagonjwa wengi wa  Kifua Kikuu na Ukoma wanapata changamoto nyingi za kiuchumi na Kijamii kwa sababu kuna mahusiano makubwa sana kati ya Kifua Kikuu, Ukoma na umasikini hivyo huu mpango unaenda kuwakinga na kuwaondolea wagojwa wetu madhira wanayoweza kuyapata kutokanayo pindi wanapougua magonjww haya, aidha mpango  unalenga kueleza huduma mbalimbali nyingine za kuwakinga ambazo zitakuwa zinafanyika kuanzia ngazi ya taifa mpaka kaya alisema.