Phone: +255 (0) 26 2960150 | Email: info@ntlp.go.tz
Home / Media / Blog / WIZARA, MIKOA TISA WAJIPANGA KUPAMBANA NA KIFUA KIKUU

WIZARA, MIKOA TISA WAJIPANGA KUPAMBANA NA KIFUA KIKUU

image

Waganga wakuu wa mikoa, waratibu wa kifua kikuu na ukoma wa mikoa na watalamu wa wizara ya Afya  watakiwa kuja na mpango wa kiutekelezaji utakaowezesha kuwaibua na kuwafikia wagonjwa wa Kifua Kikuu zaidi ya 14000 wakiwemo watoto ili kutokomeza ugonjwa huo ifikapo 2030.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Ahmed Makuwani Januari 8, 2025 Mkoani Dodoma wakati akifungua kikao Waganga wakuu wa Mikoa, waratibu wa kifua kikuu na ukoma wa mikoa na watalamu wa wizara ya Afya kujadili utekelezaji wa mpango harakishi wa uibuaji wagonjwa wa TB.

Mpango ambao unategemewa kutekelezwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya, ngazi ya jamii pamoja na makundi yaliyo katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa Kifua Kikuu hasa wachimbaji wa madini migodini, wavuvi, wajidunga na makundi mengine Ndugu Washiriki kwa Mikoa 9 Tanzania bara na halmashauri 76.

images-1.jpg

Dkt. Makuwani amesema Tanzania inaendelea kukabiliana na changamoto ya kuwapata wagonjwa wa Kifua Kikuu na kuwaweka kwenye matibabu ili kuiondoa nchi katika kundi la nchi 30 zinazochangia asilimia 87 ya wagonjwa wote wa Kifua Kikuu Duniani.

“Januari 6, 2025 Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Joakim Mhagama alizindua rasmi mpango wa kitaifa wa kuharakisha uibuaji wa wagonjwa wa Kifua Kikuu katika mikoa 9 ya Dar es salaam, Dodoma, Geita, Kagera, Mara, Simiyu, Shinyanga, Ruvuma na Tanga na kugawa mashine 185 za ugunduzi wa vimelea vya Ugonjwa wa Kifua Kikuu na alitoa maelekezo yanayolenga kuongeza juhudi za uibuaji wagonjwa wa Kifua Kikuu nchini,” amesema Dkt. Makuwani.

Dkt. Makuwani amesema, lengo ni kupunguza visa vya Kifua Kikuu kwa 50%  na vifo kwa 75% ifikapo 2025 ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2015, ambapo Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2023, Tanzania imeweza kupunguza visa vya Kifua Kikuu kwa 40%.

“Tanzania imeweza kupunguza vifo vitokanavyo na Kifua Kikuu kwa asilimia 69 kwa takwimu za mwaka 2023, ambapo lengo ni kupunguza vifo vitokanavyo na Kifua Kikuu kwa asilimia 75 mwaka 2025 ikilinganishwa na takwimu za 2015, Katika Mpango huu tunategemea kuwaibua wagonjwa wa Kifua Kikuu zaidi ya elfu kumi na nne wakiwemo watoto,” amesema Dkt. Makuwani.
Katikankuhitimisha ametoa raibkwa mikoa kubena jukumu la utekelezaji wa kampeni hiyo na kushirikiana kikamilifu na Wizara ya Afya, OR-TAMISEMI na wadau. 

images-2.jpg

“Kila mkoa umepangiwa lengo la wagonjwa, zoezi hili linategemea ushiriki wa Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ili kuhakikisha wanahamasisha wananchi kujitokeza kuchunguzwa na kupimwa ugonjwa wa Kifua Kikuu na magonjwa mengine, Niwaombe mfikishe ujumbe wa Mh. Waziri kwa Wakuu wa Mikoa na viongozi wengine za Serikali na jamii, Ninafahamu kuwa kila mkoa unaweza kuwa na mbinu na namna mahsusi ya utekelezaji. Ninaomba tuzingatie ushirikishwaji wa wadau wa mkoa, ili kupata matokeo yanayotarajiwa,,” amesema Dkt. Makuwani.