Phone: +255 (0) 26 2960150 | Email: info@ntlp.go.tz
Home / Media / Blog / WIZARA YA AFYA YAZINDUA MAPITIO YA MPANGO MKAKATI WA SITA WA KIFUA KIKUU NA UKOMA 2021-2025

WIZARA YA AFYA YAZINDUA MAPITIO YA MPANGO MKAKATI WA SITA WA KIFUA KIKUU NA UKOMA 2021-2025

image

WIZARA YA AFYA YAZINDUA ZOEZI LA MAPITIO YA KATI YA MPANGO MKAKATI WA SITA WA KIFUA KIKUU NA UKOMA 2021-2025

Dodoma.

Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma imezindua zoezi la mapitio ya kati ya Mpango Mkakati wa Sita (NSP VI 2020-2025) wa Kifua Kikuu na Ukoma. Uzinduzi wa zoezi hilo umetekelezwa na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Samuel Lazaro leo tarehe 30 Januari, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete  Jijini Dodoma. 

Matokeo ya tathmini hii yatasaidia kuboresha Mpango Mkakati wa VI katika kipindi cha muda wa utekelezaji uliobaki  wa mwaka 2023-2025 na hivyo kufikia malengo ya kitaifa na kidunia katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu na Ukoma.

Aidha , tathmini hii itasaidia pia Kutoa dira katika uandishi wa maombi ya awamu ya nne ya ufadhili wa Mfuko wa Dunia (NFM4) na Mkakati wa USAID Global TB

whatsapp_image_2023-01-30_at_16_04_35-1.jpeg

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Watathmini wa nje kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), USAID,Stop TB partnership, Watalaam Washauri Wabobezi wa Kimataifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Afya pamoja na wadau mbalimbali wa utekelezaji wa afua za Kifua Kikuu nchini. 

whatsapp_image_2023-01-30_at_16_04_37-1.jpeg

Ziara ya tathmini hiyo inaanza  kufanyika leo tarehe 30 Januari,2023 mpaka tarehe 10 februari,2023 katika mikoa 14 nchini iliyopendekezwa.