Phone: +255 (0) 26 2960150 | Email: info@ntlp.go.tz
Home / Media / Blog / DKT. MOLLEL AWAPONGEZA WATUMISHI WA PROGRAMU KWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA WELEDI.

DKT. MOLLEL AWAPONGEZA WATUMISHI WA PROGRAMU KWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA WELEDI.

image

Dodoma,

Naibu Waziri wa Afya Mhe. Godwin Mollel tarehe 27 Agosti, 2024 alikutana na watumishi wa Programu kutoka Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) pamoja na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini (NASHCoP) katika ofisi za Wizara ya Afya zilizopo kilimani jijini Dodoma.
images-1.jpg
Akiwa katika kikao kazi hicho ambacho Dkt. Mollel aliambana na Naibu Katibu Mkuu Bw. Ismail Rumatila na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt, Ahmed Makuwani aliwapongeza watumishi wa Programu hizo chini ya Mkuu wa Programu Dkt. Catherine Joachim kwa kutekeleza vizuri shughuli za kupambana na magonjwa hayo nchini.

Pia Dkt.Mollel, aliwataka watumishi wa progomu kuendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa ueledi mkubwa ili kuleta tija na ufanisi katika kufikia malengo ya nchi ya kutokomeza magonjwa haya.

Kikao hicho kiliitishwa kwa lengo la kupokea taarifa za utekelezaji na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu udhibiti wa magonjwa hayo nchini.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu aliwapongeza watumishi wa Programu hizo kwa kuwa na jitihada za kupambana na magonjwa hayo pamoja na kuwataka watumishi hao kuongeza kasi katika kuwatafuta wagonjwa wanaokosekana na kuwaweka kwenye matibabu ili kuzuia kuenea kwa magonjwa haya katika jamii.

Kwa upande wake Dkt. Catherine Joachimu aliwashukuru viongozi hao kwa kutenga muda na kukutana na watumishi wa Programu hizo hatua ambayo itaongeza hamasa na chachu kwa watumishi katika kutekeleza mikakati ya nchi ya Kutokomeza magonjwa hayo ifikapo mwaka 2030.

images.jpg