Phone: +255 (0) 26 2960150 | Email: info@ntlp.go.tz
Home / Media / Blog / Kibong'oto shirikianeni na MKUTA kutengeneza mpango kazi wa kufanyia kazi matokeo ya utafiti kwa waliowahi kuugua TB na kupona

Kibong'oto shirikianeni na MKUTA kutengeneza mpango kazi wa kufanyia kazi matokeo ya utafiti kwa waliowahi kuugua TB na kupona

image

Dodoma

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumain Nagu ameitaka Hospitali ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi ya Kibongóto kwa kushirikiana na Mtandao wa Watu Waliougua Kifua Kikuu na Kupona (MKUTA) kuhakikisha wanakuja na mpango kazi wa kufanyia kazi matokeo ya utafiti wa mwaka mmoja uliofanyika wa kuchunguza watu waliowahi kuugua kifua kikuu na kupona lakini baada ya kupona hawakufatiliwa kwa karibu.

Prof. Nagu ametoa wito huo leo jijini Dodoma katika ufunguzi wa kikao kazi cha usambazaji wa matokeo ya mwaka mmoja ambao umeweza kushirikisha watu waliowahi kuumwa Kifua Kikuu na kupona lakini baada ya kupona wakawa hawafatiliwi kwa karibu kujua maendeleo yao.

Prof. Nagu amesema kuwa wanatakiwa kuwasilisha mpango kazi kwa wizara kulingana na matokeo waliopata kutoka katika utafiti uliofanyika ili kuhakikisha wanaongeza umakini dhidi ya maambukizi ya Kifua Kikuu nchini.
00f2766c-e8e3-4f2f-a28a-4691ea2ef2bf-1.jpg
Naye Mkurungenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi ya Kibongóto iliyopo Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Leonard Subi amesema kuwa kupitia utafiti huo wameweza kupata zaidi ya watu 625 ambao walikuwa katika jamii na watu hao wamefanyiwa uchunguzi tena kuona kama hawana Kifua Kikuu.
“Katika watu 625 tulio wafanyia uchunguzi tumeweza kugundua asilimia 24 kati yao tayari walishaugua tena Kifua Kikuu na wapo katika jamii na watu nane walikuwa ni wale waliopona Kifua Kikuu sugu”, ameeleza Dkt. Subi

Hivyo ametoa rai kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kushirikisha jamii hususani katika kuwafatilia kwa ukaribu watu waliougua Kifua Kikuu na kupona ili kujua maendeleo yao katika jamii.
MWISHO