Phone: +255 (0) 26 2960150 | Email: info@ntlp.go.tz
Home / Media / Blog / WAZIRI UMMY AWATAKA WATOA HUDUMA ZA AFYA NCHINI KUTOWALIPISHA FEDHA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU KWA AJILI YA HUDUMA ZA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA KIFUA KIKUU

WAZIRI UMMY AWATAKA WATOA HUDUMA ZA AFYA NCHINI KUTOWALIPISHA FEDHA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU KWA AJILI YA HUDUMA ZA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA KIFUA KIKUU

image

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewataka watoa huduma za afya nchini kutowalipisha fedha wagonjwa wa Kifua Kikuu kwa ajili huduma za uchunguzi na matibabu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu.

Waziri Ummy ameyasema hayo mapema hii leo alipoambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Global Fund Bw. Peter Sands na ujumbe wake walipotembelea katika Zahanati ya Disunyara mkoa wa Pwani kwa ajili ya Ziara ya kikazi ya kutumbelea vituo vya utoaji huduma za afya na kuona utekelezaji wa afua mbalimbali za mapambano dhidi ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.

image_6483441-1.jpg

“Huduma za kupima na matibabu ya Kifua Kikuu ni bure, kama mtu amekuja kwa lengo la kupima Kifua Kikuu kwa kutumia X-ray na Genexpert mashine anapaswa kutolipishwa fedha yoyote kwa ajili ya huduma hizo” amesema Waziri Ummy

image_6483441_3.jpg

Aidha, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo ameridhishwa na ueledi wa watoa huduma za afya pamoja na huduma zitolewazo  na Kliniki tembezi (Mobile Clinic) ambapo ameiomba serikali kuendelea kuimarisha huduma hizo ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi wenye uhitaji wa huduma hiyo na kuweza  kufikia malengo ya kidunia ya kutokomeza Kifua Kikuu nchini Tanzania.

Waziri Ummy kwa niaba ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amelishukuru shirika la Global Fund kupitia Mkurugenzi wake kwa ufadhili wa fedha wanazotoa kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya hapa nchini.

image_6483441_2.jpg

Vilevile Bw. Sands amemshukuru Mhe. Rais kwa kumualika kuja nchini Tanzania kujionea uhalisia wa fedha wanazotoa kwa ajili ya wananchi katika utoaji wa huduma za UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria katika ngazi ya msingi na ameahidi kuendeleza uhusiano mzuri na wa muda mrefu uliopo kati yaSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Global Fund.