Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu leo amefanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Global Fund Bw. Peter Sands kuhusu uboreshaji wa huduma za afya nchini kupitia miradi ya Global Fund inayotekelezwa hapa nchini.
Read moreNaibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel amefanya kikao kazi na watumishi wa Idara ya Kinga kikiwa na lengo la kupeana taarifa za kiutendaji na kujadili muelekeo wa huduma za kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya Kifua Kikuu na Ukoma. Kikao hicho kilichofanyika katika Hospitali ya Benjamini Mkapa, Jijini Dodoma.
Read moreWizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (ECSA - HC) wameendesha mafunzo kwa Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya Serikali na binafsi kutoka nchi 12 juu ya kuandika habari sahihi kuhusu ugonjwa wa Kifua Kikuu hasa katika maeneo ya migodi.
Read moreWaziri Ummy amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Maabara hiyo iliyopo katika Hospitali ya Kibong'oto Wilayani Siha inayotegemewa kupima sampuli ya magonjwa mbalimbali ambukizi.
Read more